FUNDI:-Fundi ni mtu muhimu sa na katika swala zima la ujenzi wa nyumba yako, kwani fundi ndiye hitimishisho ya kila kitu katika ndoto yako ya mda mrefu ya kua na nyumba, hivyo usione haya kumchagua fundi bora na sio bora fundi wa ujenzi katika ujenzi wa nyumba yako.
Makazi bora na salama ni haki ya kila Mtanzania, tuhamasishane kuweza kufikia viwango bora vya makazi ya kibinadamu. Maswali mengi zaidi niliyoulizwa yanahusu ujenzi wa gharama nafuu. Wakati mwingine nasema ujenzi wa gharama nafuu ni kilio kikuu kwa Watanzania walio wengi pasipo kujali tofauti ya vipato vyao.
Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kutimiza ndoto yako ya kuwa na makazi bora kulingana na kipato chako.
- UBUNIFU WA UMBO LA NYUMBA
- ZINGATIA MAONI YA WATU (USHAURI).
- USIMAMIZI WA UJENZI WA NYUMBA (MSIMAMIZI).
- UTAWALA WA NCHI KISIASA.
Ubunifu wa majengo ni hali ya mafikirio ya kuweka umbo la taswira iliyo kwenye mfumo wake wa ubongo na kuiweka kwenye umbo halisi katika hali ya mwonekano kwa njia ya MICHORO. MBUNIFU hua ni mtu wa kwanza katika kazi ya ujenzi, mbunifu au mchoraji huwasilisha fikra zake za michoro kisanifu na hatimae michoro hyo hutumika kuumba umbo halisi kwenye uso wa dunia katika eneo husika.
JAMBO LA KUZINGATIA katika hatu ahii mbunifu na mwenye nyumba wanaitaji kua wamoja ili kumwezesha mwenye nyumba kujitathimini kujua kama hicho kinacho buniwa katika mchoro ana uwezo wa kukijenga, mchoraji asije kuchora ramani kubwa na yenye garama kuliko uwezo na mahitaji ya muhitaji wa ramani ya nyumba. katika kufikiria ujenzi wa nyumba unastahili kua makini maana katika ujenzi kuna changamoto nyingi sana lakini pia,
Ubunifu na mwonekano halisi wa nyumba yako hutafsiri gharama halisi ya nyumba yako. Zipo njia mbalimbali zinazotumika kupunguza gharama kwenye ujenzi, wakati huohuo unafikia lengo kuu la mwonekano wa nyumba uitakayo. Mfano; njia ya kupunguza idadi ya kuta za ndani, hasa zile zisizo na ulazima,au kutokuwapo kwa kuta hizo kutathiri mgawanyo wa vyumba na mpangilio wa nyumba yako
KUMBUKA KUA Mbunifu ni muhimu sana jenga nyumba bora na ya kisasa ni bora ukajenga nyumba ndogo yenye mwonekano,kuliko nyumba kubwa na ukashindwa kuimalizia, huko ni kukosa mipango bora na ukomavu katika kufanya maamuzi sahihi na ya uhakika.
2. ZINGATIA MAONI :-
Unapaswa kutambua kuwa ujenzi wa nyumba ni uwekezaji muhimu ambao haupaswi kuwianishwa na uwekezaji wowote duniani, hivyo hupaswi kupuuza hatua yoyote unayofanaya na ambayo unatarajia kuifanya katika suala nzima la ujenzi wa nyumba.Unapaswa kujipongeza kwa kila hatua uliyofikia, endelea hivyo na ifanye nyumba yako kuwa mahali bora na salama kwa kila atakayefika hapo, kwani matarajio yako ni muhimu kuyatimiza kwa ubora wa hali ya ju zaidi , na hii itatokana na umakini na kuzingatia maoni ya wataalamu wako wa ujenzi ili usije ukajikuta unafika sehemu unakwama,au unarudia kazi kwa kutokufuata ushauri tu
3. UTAWALA WA NCHI KISIASA :-
Kukua kiuchumi katika nchi yoyote ile , iwe ni kwa jamii ama mtu binafsi hutegemea maono ya watawala walioko madarakani,Ukuaji kiuchumi hudidimizwa na vipaumbele za wanasiasa pamoja na sera namikakati mibovu ya wanasiasa hao, kwa wakati husika wa wanasiasa hao. NYUMBA ni moja ya mahitaji ya lazima ya binadamu yeyote anaeishi katika uso wa dunia , kutokuwa na makazi bora na salama ni kuhatarisha uhai wa wanafamilia yote kiujumla. Hivyo kupunguza garama ya vuifaa vya ujenzi utatokana na sera bora za watawala walioko madarakani,Akiwepo mtawala mwenye machungu na ugumu wa maisha kwa watu wake ni lazima tafsiri ya maono yake yataonekana, na jitihada zake zitaleta matokeo chanya katika TAIFA na jami yote kwa ujumla.
vvifaa vya ujenzi ikiwa ni pamoja na Saruji,mabati, nondo,kokoto igae, rangi,ni malighafi muhimu katika ujenzi ambazo huzalishwa hapa hapa nchini mwetu Tanzania.
Hivyo ni rahisi serekali ikaweka mikakati ya kuwa na bei rafiki kwa Watanzania wote wa vipato vyote na hatimaye kila mmoja wetu apate unafuu wa kununua vifaa vya ujenzi na hatimae kila mtu awe na nyumba yake.Na wahusika wenye uwezo mkubwa wa kuishauri serekali yetu katika hili ni WACHUMI na kamati ya MIPANGO YA MAENDELEO.
4. ZINGATIA USHAURI:-
Unapaswa kutambua kuwa ujenzi ni uwekezaji ambao haupaswi kulinganishwa na uwekezaji wowote uliokwishatokea, hivyo hupaswi kupuuza hatua yoyote uliyokwishaifanya na ambayo unatarajia kuifanya. Kwenye ujenzi hakuna jambo dogo linalopaswa kupuuzwa, unapaswa kujipongeza kwa kila hatua uliyofikia, endelea na ifanye nyumba yako kuwa mahali bora na salama kwa kila atakayefika hapo.
Mambo hayo matatu ni miongoni mwa sababu zinazoathiri jitihada zetu za kuwa na makazi bora kwa gharama nafuu. Kutokuwa na ubunifu na usimamizi bora kabla na wakati ya ujenzi kutakuongezea gharama maradufu. Utawekewa malighafi zisizofaa na utaambiwa vitu ambavyo havipo wala havipaswi kuwapo kwenye mfumo wa ujenzi wako, huko ni kutengeneza nyumba nyingine usiyoijua. Ni hatari na hasara katika uchumi wako. Ni vema ukafanya ujenzi wako kwa uhakika na furaha kwa kutembea na mtu atakayelinda dira yako hata kukamilika kwake.
Tuendele kupeana ushauri kupitia blogi hii ya TATECH ili kufikia kilele cha mafinikio kwa kila mtanzania.
Mwandishi wa makala hi ni mbunifu wa michoro ya majumba na mshauri wa ujenzi.
Edson Jakogwasi
Kwa mawasiliano +255 683462315
Barua pepe ni: jakogwasi@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni